Usafiri Wa Kuaminika
Safirisha mizigo yako kwa haraka kwa bei nafuu kupitia kampuni ya Modell Transport Agency yenye wataalamu wenye uzoefu katika masuala ya usafirishaji.
Usafiri wa Haraka, Ili Kazi Zako Ziendelee.
Tunatambua unahitaji kufikishiwa bidhaa zako mapema ili biashara zako ziendelee. Basi hakuna kusubiri tena. Safirisha mizigo yako na Modell Transport kwa huduma ya uhakika na kuaminika.

Utaratibu Wetu Wa Kazi
Tunachukua Mzigo Wako Popote Ulipo
Tunachukua mzigo wako na kuuleta ofisini kwetu kutoka ulipo. Iwe ni Kariakoo, Bandarini au popote pale Dar es Salaam
Tunajaza Taarifa Muhimu
Tunajaza taarifa zote muhimu kuhusu mzigo wako na kuuhifadhi mahali sala kusubiri kupakiwa.
Safari Inaanza
Mara baada ya taratibu za kupakia na mambo mengine ya clearance mzigo wako utakuwa njiani kuja kwako.
Wasemavyo Wateja Wetu
Ninapokea mizigo yangu kwa wakati na ninafanya biashara zangu. Asanteni kwa huduma nzuri na Uaminifu.
Natumia Modell Transport kutoa huduma ya delivery kwa wateja wangu wa mikoa ya kati wakinunu bidhaa za jumla kwenye duka langu.
Modell Transport walikuwa wananipa taarifa ya mzigo wangu ulipofika na muda utakaonifikia. Wanajua kuwasiliana na wateja wao.
Maswali Yaulizwayo Mara Kwa Mara
Inachukua muda gani mzigo wangu kuwasili?
Kwa wateja wa mikoa ya Shinyanga na Mwanza, tegemea kupokea mzigo wako ndani ya siku zisizozidi mbili. Kwa wateja wa Dodoma unaweza kupokea mzigo wako ndani ya siku moja hadi mbili. Ikitokea uchelewashwaji tutakutaarifu sababu za kuchelewa mzigo wako.
Mawasiliano
Ofisi za Dar: 0755395787
Mwanza: 0742256867, Dodoma: 0679338840