Yapo makampuni mengi ya usafirishaji hapa dar es salaam ambayo yote yanaweza kukufikishia mzigo wako popote ulipo mkoani. Lakini utofauti unakuja katika muda utakaopokea mzigo wako, huduma kwa wateja ya kampuni husika, usalama wa mzigo na mambo mengine.

Kama mfanyabiashara au mtu binafsi unayejali usalama wa mzigo wako pamoja na ubora wa huduma ya usafirishaji, ni vyema kuwa makini pale unapochagua huduma ya usafirishaji.

Kuna mambo mengi ya kuzingatia kabla hujakubali kupeleka mzigo wako kwenye kampuni flani ya usafirishaji.

Mahali Kampuni Ilipo

Kwa hapa Kariakoo, kama kampuni ina kieneo kidogo tu basi kuna changamoto ya usalama wa mzigo wako kwani hakutakuwa na nafasi ya kutosha kuweka mizigo ya wateja. Vile vile upakiaji utasubiri hadi usiku watu wakiwa wamepungua ndio ulete gari lipaki barani.

Sisi kampuni ya Modell Transport tuna eneo kubwa la kuhifadhi mizigo yako ikiwa inasubiri kupakiwa. Siyo kama wengine wenye fremu tu wanaiita transport agency. Tuna ofisi ya kisasa na tuna timu kubwa ya watu.

Kwa usalama wa mzigo wako, ni muhimu kuchagua kampuni ambayo ina eneo kubwa na salama kwani utaweza kuingia na gari yako kuleta mzigo.

Uwepo wa kampuni Mtandaoni

Modell Transport ni moja kati ya kampuni chache sana za usafirishaji ambayo iko active mtandaoni. Wengine hawajulikani walipo. Sisi tumerahisisha njia za mawasiliano na wateja wetu kwani tunapatikana Instagram, Facebook, tuna website yetu na pia tupo kwenye ramani ya google.

Hivyo ni rahisi sana ukiingia mtandaoni kutafuta transport agecny kukutana na sisi. Hii inakupa kuamini kwamba kweli kampuni ipo na iko serious na kazi.